• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Livestock na Fisheries
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondary
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Mipango Mija na Maendeleo ya Ardhi
      • Afya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba za Vikao
      • Vikao vya Waheshimiwa
      • Kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ya Sasa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Picha za Video
    • Hotuba Mbalimbali
    • Picha

RC Makalla aipongeza Kigamboni kwa Hati safi miaka 5mfululizo

Posted on: June 28th, 2022


Mkuu wakoa wa Dar es Salaam Mhe.Amosi Makalla ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa kuendelea kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo na kuwataka kuendeleza mwenendo huo.

Mhe. Makalla ametoa pongezi hizi kwenye kikao cha Baraza maalumu la kupitia hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwenye ukumbi wa Manispaa  na kusema kuwa Halmashauri imejitahidi kuwa na hoja chache kwa mwaka 2021 kwani nyingi zilizopo  ni za kipindi cha nyuma  ambapo kati ya hoja 43, hoja 20 zimejibiwa na 23 zilizobaki  kuhakikisha zinafanyiwa  kazi kama ilivyoelekezwa.

Ameongeza kwa kusema kuwa pamoja na hati safi uongozi unapaswa kujikita katika kudhibiti upotevu wa mapato, kutumia asilimia 70 kwenye miradi ya maendeleo, kutumia asilimia 10 ya makundi maalumu na kutambua kuwa mwaka wa fedha ujao Serikali imeongeza asilimia 15 ya ukusanyaji mapato.

"Hatupaswi kutegema Serikali Kuu katika kutekeleza miradi wakati Halmasuari inao uwezo wa kukusanya mapato, tuhakikishe tunakusanya na kudhibiti upotevu wa mapato" Alisema Mkuu wa Mkoa.

Aidha Mkuu wa Mkoa amegiza uongozi wa Manispaa kudhibiti biashara holela  kwa wafanyabiashara  kufanya kazi kwenye maeneo rasmi na kutunga sheria ndogo zinatazotumika kusimamia , kulipa fidia kwa wale wanaodai, kulinda maeneo kwa kuwekea mipaka, kudhibiti migogoro ya ardhi, kuondoa malalamiko kwa wananchi juu ya dhuluma ziazofanywa na kampuni zinazouza ardhi  kwa kuhakikisha wanafuata taratibu ili kuweze kuwahudumia Wananchi.

Pia Mkuu wa Mkoa amezielekeza  Taasisi zote zenye umiliki wa maeneo Kigamboni kuhakikisha wanasafisha maeneo yao na kuyawekea mipaka  ili kuondoa mapori kwani Kigamboni ndilo eneo pekee Dar es Salaam lililobaki kwa kuendeleza ujenzi hivyo si vyema kuwa na mapori.

 Kuhusu utekelezaji wa Anwani za makazi awamu ya Pili  ya kuweka vibao kwenye Nyumba na Barabara Mkuu wa Mkoa ameipongeza Kigamboni kwa kuendeleza vyema na kuwataka kumaliza zoezi  vizuri huku wakiendelea kuhamasisha wananchi juu ya Sensa.

Mkuu wa Mkoa alitumia fursa hiyo pia kuwakumbusha wananchi juu ya zoezi la usafi linalofanyika kila mwisho wa mwezi na kusema kuwa kila mmoja aone anajukumu la kusafisha eneo lake kuanzia ngazi ya Kaya hadi kwenye maeneo ya kazi na biashara.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangassa  amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa pongezi, kupokea maelekezo na kusema kuwa atahakikisha  yote yanafanyiwa kazi  ambavyo ameelekeza kwa kulenga kuongeza tija kwa maendeo ya Kigamboni ili kuweza kufikia malengo ya Serikali.

Angel Mosha Kaimu Mkaguzi Mkazi akiwsilisha taarifa za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuipongeza Kigamboni kwa kupata hati safi.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akiipongeza Manispaa ya Kigamboni na kutoa maelekezo ya kufanyiwa kazi wakati wa kikao cha baraza maalumu . 


Kuanzia kushoto ni Mkuu wa Wilaya Mhe. Fatma Nyangassa, Mkuu wa Mkoa Mhe. Amosi Makalla na Naibu Meya Mhe. Stephano Waryoba wakifatilia uwasilishwaji wa taarifa .


Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almas Nyangassa akipokea maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa.


Baadhi ya madiwani wakifatilia uwasilishaji wa taarifa.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg.Erasto Kiwale akitolea ufafanuzi wa hoja zilizotolewa na Madiwani wakati wa upokeaji wa taarifa za hoja za  Mkuguzi Mkuu wa Hesabu  wa Serikali

Baadhi ya Wataalamu wa Manispaa ya Kigamboni wakifatilia uwasilishaji wa taarifa ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali.


Kaimu Mkuu wa Idara ya Fedha  Genoveva Meshi akitoa taarifa fupi ya Hoja za Serikali.


Baadhi ya Madiwani wakifatilia uwasilishwaji wa taarifa ya Hesabu za Serikali kwenye mkutano wa Baraza maalumu.

Matangazo

  • Namba za simu za Wakuu wa Idara Manispaa ya Kigamboni July 04, 2022
  • Tangazo la kuitwa kazini July 12, 2022
  • Tangazo la kuitwa kazini July 12, 2022
  • Tangazo la kuitwa kazini July 12, 2022
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI TAMASHA LA HAMASA YA SENSA YAWIVA

    August 11, 2022
  • JUHUDI ZA RAIS WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA KUINUA UTALII ZAUNGWA MKONO

    August 09, 2022
  • JUHUDI ZA RAIS WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA KUINUA UTALII ZAUNGWA MKONO

    August 09, 2022
  • WAJUMBE WA MENEJIMENTI YA MANISPAA YA KIGAMBONI WAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAIA

    August 07, 2022
  • Angalia Zote

Video

RC Makalla aipongeza Kigamboni kwa Hati safi miaka 5 mfululizo
Video zingine

Kurasa za karibu

  • Municipal councilors
  • Kigamboni Municipal History
  • Investment Opportunities
  • Fomu ya Maombi ya Kiwanja
  • Huduma za Afya na Orodha ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni

    Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam

    Simu: +255222928468

    Simu ya Mkononi: +255222928468

    Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa