Wakazi wa Wilaya ya Kigamboni wanapata huduma ya maji kutoka kwenye vyanzo vya visima virefu vya Serikali 83. Kati ya hivyo visima 26 ni vya jamii, visima 57 ni vya taasisi za Serikali (31 shule ya msingi, 17 vituo vya afya na 9 shule za Sekondari). Aidha vyanzo vya maji vingine ni visima vya watu binafsi.
Mahitaji halisi ya maji ni kiasi cha lita za ujazo 15. 6 millioni kwa siku (wastani wa lita 80 kwa mtu kwa siku). Kiasi halisi cha uzalishaji wa visima vya serikali inakadiriwa kuwa ni lita za ujazo 8.97 millioni kwa siku. Sawa na asilimia 51.1
Katika kukabiliana na upungufu wa maji na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama Serikali kupitia mamlaka ya maji safi na maji Taka (DAWASA), visima virefu 15 kati ya visima ishirini (20) vimechimbwa katika kata za Kimbiji na Kisarawe II. Mara mradi huu utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita za ujazo 270 milioni.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kupitia Programu ya maji imechimba visima virefu vitatu (3) katika kata za Vijibweni, Somangila na Pemba Mnazi. Visima hivi vinauwezo wa kuzalisha maji lita za ujazo 264,000.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa